Nenda kwa yaliyomo

Cesc Fabregas

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 14:16, 10 Septemba 2017 na Eltonder (majadiliano | michango) (Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ''''Francesc "Cesc" Fabregas Soler''' ni mchezaji anayetokea nchini Hispania alizaliwa tarehe 4 Mei 1987 mji wa Arenys De Mar.Anachezea [[Premier League]...')
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)

Francesc "Cesc" Fabregas Soler ni mchezaji anayetokea nchini Hispania alizaliwa tarehe 4 Mei 1987 mji wa Arenys De Mar.Anachezea Premier League kwa sasa klabu ya Chelsea nafasi ya kiungo wa kati na timu ya taifa ya Hispania. Fabregas alitokea La Masia,akademi ya Barcelona aliacha akademi hiyo akiwa na miaka 16 na kusajiliwa na klabu ya Premier League ya Arsenal September 2003.Baada ya viungo wa timu hiyo kupata majeraha alipata nafasi ya kuonyesha uwezo wake katika msimu wa 2004-05 na alifanikiwa kuzuia mipango ya timu pinzani na kuibuka mchezaji bora katika nafasi yake na kushinda kombe la FA mwaka 2005.Baada ya hapo alihamishwa na kurudishwa tena Barcelona kwa £35 kutoka London Agosti 15 2011.Kwa miaka mitatu aliyokaa Camp Nou alicheza pembeni ya Xavi na Iniesta na kufanikiwa kushinda mataji kama La liga,Klabu Bingwa ya Dunia,Copa Del Rey,UEFA Super Cup,na Spanish Super Cup.Na June 2014 alirudi tena London Kwenye klabu ya Arsenal kabla ya uhamisho wa kwenda Chelsea kwa ada ya £30.Na katika ngazi ya timu ya taifa Fabregas alianza kucheza mwaka 2006 na kuiwakilisha nchi yake kwenye 2006 FIFA World Cup, UEFA Euro 2008, 2009 FIFA Confederations Cup, 2010 World Cup, Euro 2012, 2013 Confederations Cup, the 2014 World Cup and Euro 2016 Kwenye mashindano ya European Championship Fabregas aling'ara sana na kuwa chanzo cha ushindi 2008 na 2012 na mwaka 2010 ndiye aliyetoa pasi kwa Andres Iniesta iliyozaa goli kwenye fainali ya kombe la dunia alipata kepu yake ya 100.