Nenda kwa yaliyomo

Oreste Baratieri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 12:46, 20 Septemba 2006 na Kipala (majadiliano | michango)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)

Oreste Baratieri 13 Novemba 1841-7 Agosti 1901) alikuwa jenerali katika jeshi la Italia na gavana wa koloni ya Eritrea aliyeongoza Waitalia katika mapigano ya Adowa waliposhindwa vibaya na Ethiopia.

Baratieri alikuwa mwenyeji wa jimbo la Tirol katika kaskazini ya Italia. Alishiriki katika mapigano ya vita ya maungano ya Italia chini ya Guiseppe Garibaldi 1860 / 1861.

1891 alipewa cheo cha jenerali na kuwa mkuu wa jeshi la Italia katika Eritrea. 1892 alikuwa pia gavana. Baratieri aliongoza wanajeshi wake katika ushindi wa mapigano mbalimbali dhidi ya vikosi vya watemi na makabila ya Ethiopia.

1895 alipokea amri za serikali yake ya kushambulia Ethiopia baada ya Negus Menelik II alikana mkataba wa Wuchale. Baratieri alitembelea Italia na kuwahutubia wanachi akiwaahidi atamleta Menelik kama mfungwa.

Oktoba 1895 Baratieri alivuka mto Mareb na kuingia Ethiopia. Baada ya mapigano ya kwanza alijifunza kuhusu jeshi kubwa la Menelik akaamua kusubiri hadi akiba za chakula cha Waethiopia ziishe. Lakini serikali ya waziri mku Crispi alitaka kutangaza ushindi ikamwamuru Baratieri ashambulie mara moja.

Shindikizo hili lilisababisha mapigano ya Adowa ambako wanajeshi 17,000 Waitalia na Waeritrea walipigwa vibaya na jeshi la Menelik lenye wanajeshi kati 80,000 hadi 100,000. Waitalia walipoteza wanajeshi 10,000 waliokufa au kutekwa wafungwa na adui pamoja na mizinga yote na bunduki 11,000. Wengine waliweza kukimbia na kujiokoa katika Eritrea.

Baratieri aliweza kujiokoa lakini alisimamishwa mbele ya mahakama ya kijeshi iliyoona ya kwamba alifanya makso lakini hana hatia. Mwaka 1897 alijiondoa madarakani na kuchukua pensheni yake. Aliishi katika Tirol ya Kiaustria alipoaga dunia tarehe 7 Agosti 1901 mjini Sterzing-Vipiteno.