Nenda kwa yaliyomo

Ziwa Eyasi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

3°35′S 35°0′E / 3.583°S 35.000°E / -3.583; 35.000

Ziwa Eyasi kutoka angani.

Ziwa Eyasi (zamani pia Ziwa Njarasa, au Ziwa Hohenlohe) ni ziwa la chumvi kubwa nchini Tanzania linalopatikana katika Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha. Liko upande wa kaskazini mwa Tanzania, kusini kidogo mwa Hifadhi ya Serengeti, mita 1,030 juu ya usawa wa bahari.

Ziwa Eyasi ndio chanzo kikubwa cha maji mkoani Arusha. Ni ziwa la msimu la maji chumvi, lenye kina kirefu kwenye sakafu ya Bonde Kuu la Ufa la Afrika Mashariki. Ziwa limeinuliwa na kuelekezwa kusini-magharibi hadi kaskazini-mashariki mwa Tanzania, na liko katika tawi la Eyasi-Wembere la Bonde Kuu la Ufa.

Eyasi ni ziwa lenye upepo mkali sana, labda kuliko maziwa yote nchini Tanzania, kwani unavuma saa 24 bila kutulia hata baadhi ya wavuvi wakubwa (wengine kutoka ziwa Nyasa, wengine kutoka ziwa Viktoria) wanashindwa na upepo, mpaka wanakimbia ziwa hilo na kwenda ziwa jirani la Manyara.

Wahadza ndio wakazi asilia wa ziwa hilo. Wanapatikana katika eneo kubwa karibia eneo hilo lote.

Pango la Mumba ni kituo cha kiakiolojia ambacho kiko kando ya Ziwa Eyasi.

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Arusha bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ziwa Eyasi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.