Nenda kwa yaliyomo

Ericsson

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sony Ericsson T630.

Ericsson ni kampuni ya teknolojia ya mawasiliano iliyoanzishwa mwaka 1876 na Lars Magnus Ericsson. Kampuni hii inatoka nchini Sweden na ilianza kama karakana ya vifaa vya simu huko Stockholm. Ericsson imekuwa ikifanya kazi kwa muda mrefu katika sekta ya teknolojia ya mawasiliano.

Mwaka wa 2001, Ericsson iliungana pamoja na Sony wakaunda Sony Ericsson, chini ya mwamvuli wa Sony Corporation. Muungano huu ulikuwa na shabaha ya kuunganisha nguvu za Ericsson katika teknolojia ya mawasiliano na Sony katika sekta ya elektroniki ya watumiaji, hasa simu za mkononi. Hata hivyo, mwaka 2012, Sony ilinunua hisa zote za Ericsson na hivyo kumaliza ushirikiano huo, na kubadili jina la kampuni hiyo kuwa Sony Mobile Communications.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]


Makala hii ni sehemu ya mradi wa kuboresha Wikipedia na Wikamusi ya Kiswahili. Unaweza kusaidia kuihariri na kuongeza habari.